Thursday, January 03, 2008

MNAMPATA HUYU MSELA WATU WANGU?

Jamaa ni muigizaji mkali sana toka Hollywood,Jina lake kamili na Mark Alan Dacascos, alizaliwa tarehe 26 February 1964, Honolulu, Hawaii, USA. Baba yake anaitwa Al Dacascos ni Mfilipino, mama yake mzazi anaitwa Moriko McVey, lakini Mark alilelewa na mama wa kambo aliyeitwa Malia Bernal. Alianza kupata ushindi wa karate na kung fu akiwa na umri wa kati ya miaka 09 na 18. Mark ameoa, mke wake anaitwa Julie Condra na ana mtoto mmoja anaitwa Makoa Dacascos ambae alizaliwa tarehe 31 December 2000, Oahu, Hawaii, USA.Kama kawaida wahenga wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, Dogo anaonekana atafuata nyayo za baba yake maana hadi sasa amekwisha igiza filamu inayoitwa Final Approch (2006). Mark Dacascos mweyewe amekwisha igiza filamu(movie) nyingi sana kama vile American Samurai(1992), Only the strong(1993), Crying Freeman(1995), Drive(1997), Final Approach(2006), Code Name.The Cleaner(2007), I am Omega(2007), The Legend of Bruce Lee ambayo inatoka April mwaka huu 2008.Jamaa ana movie kibao.Mark anaongea lugha ya kiingereza, kijerumani na kimandarin, pia viywaji vyake ni maji na chai tu. Mark amekwisha wahi pata tuzo ya Saturn Award mwaka 2002.Kwa ujumla Mark Dacascos ni muigizaji mkali sana, tafuta na uangalie movie yake yoyote ile na utakuja niambia mwenyewe.Pia unaweza kubofya hapa ili kupata mambo mengine ya Mark. Msikose kufuatili mambo mengine kama haya yaani ni Utamuu! Ciao!!!
Pamojaa.






1 comment:

Anonymous said...

Ebwana kweli jamaa anatisha,
Vipi tabia zake akiwa mtaani ndo hivyo hivyo au?

Ebwana umeshacheki kitu kinakwenda kwa jina la "Cradle to the Grave" yuko na Jet Li yani ni hakuna ku blendi kwasababu vumbi linalotimka hapo usi paime kabaisa.

Keep it up m2wangu