Thursday, January 03, 2008

MNAMPATA HUYU MSELA WATU WANGU?

Jamaa ni muigizaji mkali sana toka Hollywood,Jina lake kamili na Mark Alan Dacascos, alizaliwa tarehe 26 February 1964, Honolulu, Hawaii, USA. Baba yake anaitwa Al Dacascos ni Mfilipino, mama yake mzazi anaitwa Moriko McVey, lakini Mark alilelewa na mama wa kambo aliyeitwa Malia Bernal. Alianza kupata ushindi wa karate na kung fu akiwa na umri wa kati ya miaka 09 na 18. Mark ameoa, mke wake anaitwa Julie Condra na ana mtoto mmoja anaitwa Makoa Dacascos ambae alizaliwa tarehe 31 December 2000, Oahu, Hawaii, USA.Kama kawaida wahenga wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, Dogo anaonekana atafuata nyayo za baba yake maana hadi sasa amekwisha igiza filamu inayoitwa Final Approch (2006). Mark Dacascos mweyewe amekwisha igiza filamu(movie) nyingi sana kama vile American Samurai(1992), Only the strong(1993), Crying Freeman(1995), Drive(1997), Final Approach(2006), Code Name.The Cleaner(2007), I am Omega(2007), The Legend of Bruce Lee ambayo inatoka April mwaka huu 2008.Jamaa ana movie kibao.Mark anaongea lugha ya kiingereza, kijerumani na kimandarin, pia viywaji vyake ni maji na chai tu. Mark amekwisha wahi pata tuzo ya Saturn Award mwaka 2002.Kwa ujumla Mark Dacascos ni muigizaji mkali sana, tafuta na uangalie movie yake yoyote ile na utakuja niambia mwenyewe.Pia unaweza kubofya hapa ili kupata mambo mengine ya Mark. Msikose kufuatili mambo mengine kama haya yaani ni Utamuu! Ciao!!!
Pamojaa.






Tuesday, January 01, 2008

MWAKA MPYA NDIO HUU!

Kwanza hatuna budi kumshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kutupenda sisi mpaka kufikia mwaka huu mpya ni lazima tumshuru kwa kutuweka hai hadi leo hii tanaendelea kupumua pumzi yake ya bure, pia bila kusahau ana makusudi nasi basi tumtumikie na kushika amri zake. Kama nilivyokwisha watakia heri nyingi za mwaka huu mpya na bado nawatakia tena na tena.
Basi kama kawa na mwaka huu nitaendelea kuwapa mambo kibao mazuri yanayohusu movie pamoja na waigizaji.Pamojaa.

Monday, December 31, 2007

HUYU HAPA BRAD PITT MTU WANGU.

Watu wangu poleni sana kwa kusubiri kwa muda mrefu kidogo,lakini najua mnafahamu mambo ya sikukuu.kama mnavyojua wiki ya mwisho wa mwaka huwa karibu yote ni pilika za sikukuu.Tuyaache hayo.
Kama nilivyokuwa nimewaahidi lazima nitawaletea history ya muigizaji maarufu na mkali kutoka Hoollywood na huyu si mwingine ni Brad Pitt.
Kama nlivyowaambia mwanzo wakati nawapa story ya Angelina, hawa ni watu wilioowana na raha zaidi wanaigiza wote, check movie zao zimetulia.
Kwa kuanza jina kamili la huyu mshikaji ni William Bradley Pitt,alizaliwa tarehe 18 December 1963,Shawnee, Oklahoma, USA. Mama yake anaitwa Jane Etta Hillhouse na baba yake William(bill) Pitt. Pia kabla ya kuwa na Angelina alikuwa na mke wake aliyeitwa Jennifer Aniston ambae alimuoa tarehe 29 July na kumtaliki tarehe 02 October 2005 na ndipo alipo muoa Ange.Pamoja na kuwa muigizaji pia ni mtayarishaji wa filam,Jamaa alianza kupata umaarufu wake katika miaka ya tisini.Kama kawaida ameigiza movie kibao sana lakini ni baadhi ni kama Troy 2004, Mr& Mrs smith 2005, Babel 2006, Ocean Thirteen 2007 na zingine nyingi.Jamaa ana Historia ndefu sana ili nisiwachoshe pata hii kwa ufupi kabisa na usikose kufatilia issue kama hizi kibao za huyu na wengine. NAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2008. Tchaooo.