Saturday, February 23, 2008

MUDA KIDOGO LAKINI TUPO PAMOJA


Mambo yanakwendaje watu wangu? ni muda kidogo sijapanda hewani lakini hii ni kwa sababu ya matatizo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wangu lakini namshukuru Mungu kwa kuwa yeye ndio kila kitu. Lakini msijali sana maana kwa uweza wake bado tupo pamoja na tutaendeleza jahazi hili.
Endelea kucheck blog hii. Pamojaa!



Thursday, January 31, 2008

MAMBO SHWARIIII?

Ebwana issue zinakwendaje? Habari za muda kidogo. Mambo yamebana kidogo lakini muda si mrefu tutakuwa pamoja kama kawaida na mtaendelea kupata mambo mazuri.

Sunday, January 20, 2008

KUTOKA MIELEKA MPAKA FILAMU(MOVIE)


Unampata huyu jamaa? kwa kifupi kabisa mshikaji alikuwa bonge la superstar kwenye WWE lakini kwa sasa jamaa amegeuka upande mwingine sasa ni bonge la muigizaji (actor) jamaa anatisha na hadi sasa ana movie kibao. Usikose historia yake kwa kirefu kabisa hapa hapa ndani ya blog hii.

Friday, January 18, 2008

MMEIPATA HII??


Ebwana mmeipata hii msella wetu ambae ni bonge la muigizaji hapa Tanzania, Steven Kanumba sasa anajiita a.k.a Denzel Wshington wa Bongo (Tz), jamaa ametembelea Hoolywood, Marekani ambayo n i sehemu inayoongoza kwa mambo ya filamu diniani kote. Kanumba akiwa Hoolywood ametembelea studio kadhaa kama vile Warner Brothers na Universal studios.Tunamtakia mafanyikio makubwa sana Kanumba kwa sio tu kwamba atajitangaza yeye lakini pia ataitangaza nchi yetu ya Tanzania na kujulikana katika ulimwengu wa filamu.Nashukuru sana blog ya swahilitime.blogspot.com pia unaweza kwenda kwa kuangalia picha na habari zaidi za Kanumba.








Tuesday, January 15, 2008

HEY!! MAMBO VIPI TUPO WOTE?

Mambo yanakwendaje watu wangu wote nadhani shughuli zinaendelea kama kawaida. Mishangae sana kwa kutokuwa hewani kwa muda kidogo na matizo na mambo mengine ambayo yalifanya kuwa busy kidogo.Lakini msihofu siku zote tutakuwa pamoja ili kupeana mambo matamu ya movie pamoja na waigizaji au sio? Msikonde tupo pamojaa.

Thursday, January 03, 2008

MNAMPATA HUYU MSELA WATU WANGU?

Jamaa ni muigizaji mkali sana toka Hollywood,Jina lake kamili na Mark Alan Dacascos, alizaliwa tarehe 26 February 1964, Honolulu, Hawaii, USA. Baba yake anaitwa Al Dacascos ni Mfilipino, mama yake mzazi anaitwa Moriko McVey, lakini Mark alilelewa na mama wa kambo aliyeitwa Malia Bernal. Alianza kupata ushindi wa karate na kung fu akiwa na umri wa kati ya miaka 09 na 18. Mark ameoa, mke wake anaitwa Julie Condra na ana mtoto mmoja anaitwa Makoa Dacascos ambae alizaliwa tarehe 31 December 2000, Oahu, Hawaii, USA.Kama kawaida wahenga wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, Dogo anaonekana atafuata nyayo za baba yake maana hadi sasa amekwisha igiza filamu inayoitwa Final Approch (2006). Mark Dacascos mweyewe amekwisha igiza filamu(movie) nyingi sana kama vile American Samurai(1992), Only the strong(1993), Crying Freeman(1995), Drive(1997), Final Approach(2006), Code Name.The Cleaner(2007), I am Omega(2007), The Legend of Bruce Lee ambayo inatoka April mwaka huu 2008.Jamaa ana movie kibao.Mark anaongea lugha ya kiingereza, kijerumani na kimandarin, pia viywaji vyake ni maji na chai tu. Mark amekwisha wahi pata tuzo ya Saturn Award mwaka 2002.Kwa ujumla Mark Dacascos ni muigizaji mkali sana, tafuta na uangalie movie yake yoyote ile na utakuja niambia mwenyewe.Pia unaweza kubofya hapa ili kupata mambo mengine ya Mark. Msikose kufuatili mambo mengine kama haya yaani ni Utamuu! Ciao!!!
Pamojaa.






Tuesday, January 01, 2008

MWAKA MPYA NDIO HUU!

Kwanza hatuna budi kumshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kutupenda sisi mpaka kufikia mwaka huu mpya ni lazima tumshuru kwa kutuweka hai hadi leo hii tanaendelea kupumua pumzi yake ya bure, pia bila kusahau ana makusudi nasi basi tumtumikie na kushika amri zake. Kama nilivyokwisha watakia heri nyingi za mwaka huu mpya na bado nawatakia tena na tena.
Basi kama kawa na mwaka huu nitaendelea kuwapa mambo kibao mazuri yanayohusu movie pamoja na waigizaji.Pamojaa.