Monday, December 31, 2007

HUYU HAPA BRAD PITT MTU WANGU.

Watu wangu poleni sana kwa kusubiri kwa muda mrefu kidogo,lakini najua mnafahamu mambo ya sikukuu.kama mnavyojua wiki ya mwisho wa mwaka huwa karibu yote ni pilika za sikukuu.Tuyaache hayo.
Kama nilivyokuwa nimewaahidi lazima nitawaletea history ya muigizaji maarufu na mkali kutoka Hoollywood na huyu si mwingine ni Brad Pitt.
Kama nlivyowaambia mwanzo wakati nawapa story ya Angelina, hawa ni watu wilioowana na raha zaidi wanaigiza wote, check movie zao zimetulia.
Kwa kuanza jina kamili la huyu mshikaji ni William Bradley Pitt,alizaliwa tarehe 18 December 1963,Shawnee, Oklahoma, USA. Mama yake anaitwa Jane Etta Hillhouse na baba yake William(bill) Pitt. Pia kabla ya kuwa na Angelina alikuwa na mke wake aliyeitwa Jennifer Aniston ambae alimuoa tarehe 29 July na kumtaliki tarehe 02 October 2005 na ndipo alipo muoa Ange.Pamoja na kuwa muigizaji pia ni mtayarishaji wa filam,Jamaa alianza kupata umaarufu wake katika miaka ya tisini.Kama kawaida ameigiza movie kibao sana lakini ni baadhi ni kama Troy 2004, Mr& Mrs smith 2005, Babel 2006, Ocean Thirteen 2007 na zingine nyingi.Jamaa ana Historia ndefu sana ili nisiwachoshe pata hii kwa ufupi kabisa na usikose kufatilia issue kama hizi kibao za huyu na wengine. NAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2008. Tchaooo.

Friday, December 28, 2007

MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR!

Samahani sana watu wangu si mnajua mambo ya christmas,Lakini msikonde bado tupo pamoja kama kawaida.Nawatakia sikukuku njema japo nimechelewa kidogo lakini natumaini imekwenda fresh. Pia nawatakia heri ya mwaka mpya wa 2008 tumuombe Mungu atusaidie tufike salama, Amen. Kuhusu mambo yote niliyo waahidi yote yatakwenda kama yalivyopangwa tuombeane uzima.Pamoja na hayo kuna kitu tofauti sana cha ukweli najua wote mtafurahi kama mnavyoenjoy hii bonyeza hapa. Pamoja Tchaooo.

Sunday, December 23, 2007

EBWANA KAMA KAWAIDA!

Watu wangu mambo vipi?Ile issue ya Pitt msikonde ntawapandishia muda si mrefu naomba mniwieradhi kuna mambo yamenibana lakini tupo pamoja kama kawa.Sorry sana mshikaji wangu nard, Halafu blog yako huwa naifungua Bro vipi mbona hupandishi vitu napenda sana kuwa naisoma.Pamoja!!

Thursday, December 20, 2007

HII NI KWA WOTE AU SIOO?

Kutokana na yale maombi niliyowaambia hapo awali huyu alikuwa anataka kujua historia ya waigizaji Angelina Jolie na brad Pitt.Kwa kifupi kwanza hawa ni mtu na mme wake.Leo ntakupa mambo muhimu ya Angelina na baadae Pitt.

Angelina Jolie Voight hilo ndilo jina lake kamili alizaliwa June 04,1975 Los Angeles,California USA.Baba yake anaitwa Jon Voight na mama yake Marcheline Bertrand.Pamoja na kuwa muigizaji wa muda sana pia alikuwa mwanamitindo.Angelina pia ni balozi wa umoja wa mataifa(UN)katika mambo ya wakimbizi.Anajulikana kwa majina mengine(Nickname) kama Angie,Catwoman,Ange&AJ.Angie ameigiza movie nyingi sana lakini baadhi ni Tomb Raider 2001&2003,Alexander 2004,Mr&Mrs Smith 2005,The Good Shepherd 2006,A Mighty Heart 2007 na mpya inayotamba sasa Beowulf 2007.Pia kuna baadhi ambazo zitatoka 2008 kama Kung Fu Panda,Wanted na zingine.Angeline ameshinda tuzo kama Showest 2000,Oscar 1999 na zingine nyingi tu.Ana mambo kibao lakini kwa ufupi ni hayo.Usikose issue za Brad Pitt.

WATU WANGU MNIWIE RADHI

Kwanza kabisa nilikuwa nataka kuwaomba msamaha watu kwa kutokuwa hewani kwa siku kazaa lakini kama nilivyowaambia tupo pamoja.Hii pia ni pamoja na mtu ambaye alikuwa anitaka kujua historia ya waigizaji maarufu huko Hoollywood,Mshikaji wangu nakwambia leo hii nitakupa vitu.Pia waweza kucheki hapa ili kupata vitu na nilipotolea maoni hayo.

Friday, December 14, 2007

CHEZA SALAMA.

Unamcheki huyo hapo?Jamaa anacheza na nyoka si kitoto,huyo ni msela wangu toka Moshi, jamaa anapenda movie.Je anaweza kuwa muigizaji wa movie za kutisha kwa kuonesha ujasiri wake au wewe unasemaje?

Monday, December 10, 2007

MAMBO SHWARII?

Ebwana mambo vipi watu wangu msikonde nawaandali vitu vya maana msikose au sio?

Thursday, December 06, 2007

WAMJUA SALMA HAYEK WEWE MPWA WA OSAMA?

Huyu ni muigizaji mzuri na maarufu sana wa kike aliyejichukulia umaarufu mkubwa sana huko Hoolywood.Salma alizaliwa tarehe 02 september 1966, Coatzacoalcos, Veracruz, Mexco. Sasa ana umri wa miaka 41, na jina lake kamili ni hilo hilo Salma Hayek Jimeneaz.Mwana dada huyu ameigiza movie nyingi sasa ambazo kiukweli mimi mwenyewe nazikubali, Movie za 2007 ni kama Ugly Betty na Across the Universe.Movie zake ambazo hadi sasa zinatarajiwa mwaka 2008 ni Keep Coming Back na South of the Border na pia kuna pre-production zake za 2009 inaitwa Banda,La.Pia kuna tetesi kuwa Salma ni mpwa wa Osama Bin Laden,lakini pia inadaiwa kuwa ajawahi kuonana uso kwa uso na mjomba ake huyo. Usikose mambokibao yanakuja kama kawaida.

Wednesday, December 05, 2007

UNAMJUA MGUMU AMBAYE NI MCHESHI SANA?

Najua utakuwa unajiuliza maswali mengi sana kichwani mwako huyo ni nani haswa? Basi kama kawaida mtu wangu hapa ndo umefika. Jamaa ni boge la actor(muigizaji) ambaye ukiangalia movie zake za comedy(ucheshi) hautaacha kufurahi mwanzo mpaka mwisho na ikibidi waweza rudia tena kuangalia.Anajulikana kwa jina maarufu kama ICE CUBE pia ana majina mengine kama Westside Connection,N.W.A, Mshikaji amezaliwa tarehe 15 June 1969,Los Angeles,California,USA.Ice Cube pia ni rapper mkali sana toka miaka mingi jamaa amekuwa akifanya HipHop. Pia Ice ni mwandishi wa mashairi na mwongozaji wa filamu.Jina la kuzaliwa la Ice Cube ni O'Shea jackson.Ana movie nyingi sana lakini movie yake inayozungumziwa ni Are We Done Yet? amboyo ni ya mwaka huu 2007.Endelea kucheki na hii tovuti utazidi kupata vitu vingi vya Ice Cube na mastar wengine kibao.

Tuesday, December 04, 2007

WAZIJUA TOP 5 ZA MOVIE.COM ZA LEO

Hizi ni TOP 5
1.Enchanted
2.This Christmas
3.Beowulf
4.Awake
5.Hitman
Hizo ndio zinabamba kwenye box-office results ya movie.com

TUPO PAMOJA?

Hii nilikuwa nataka kuwa kumbusha wale wadau na wa wapenzi wa filamu hasa katika nchi zetu ambazo ndio kwanza zinaanza kuchipukia katika mambo ya filamu,tuwaunge mkono wasanii wetu kwa kununua kazi zao.Na pia kuwapinga na kuwafichua wale wachache wanao warudisha nyuma kwa kuwaibia wasanii kazi zao.

Monday, December 03, 2007

USIKONDE MTU WANGU.

Watu wangu wote ambao tupo pamoja msiwe na tabu kabisa kama unataka kumjua star mojawapo wa movie unaweza kunitumia maoni yako nami bila hiana ntakupa mambo pamoja na kila kitu.Basi waweza nitumia maoni na kumchagua star yeyote anayetaka kujua undani wake.Shwariii!

INAPENZA SANA AU SIO WATU WANGU?

Mwisho wa wiki iliyopita nilipata bahati ya jusikiliza mahojiano ya waigizaji maarufu a hapa Bongo(Tanzania) katika kituo kimoja maarufu pia hapa kwetu Tz cha television.Nilifurahi sana kusikia toka kwao wakisema sasa afadhali hata filamu zoa za kibongo afadhali zimeanza kuwalipa waigazaji hao.Ni jambo la faraja sana maana hio inamaanisha watanzania na watu wao wa jirani wameanza kupata muamko na fleva za movie za bongo. Hii pia ni pamoja na kuanza kupata majibu kwa maswali mengi tuliyokuwa tunajiuliza, pia waweza rudia mada iliyopita.Ushauri wa bure kutoka kwangu kwa wasanii hao wasibweteke na mafanikio hayo waliyo anza kuyapata tunahitaji sana na wao wajulikane kimataifa ili watuwakilishe kwa sana au sio?

Friday, November 30, 2007

JE TUFANYAJE??

Mambo vipi watu wangu popote mlipo?Hilo swali nimelitoa kwenu ili tupate kujadili kuhusu jinsi ya kukuza soko la filamu sana sana katika nchi hazijapata maendeleo kivile.Kwa mfano mimi ni Mtanzania,na ukimuuliza Mtanzania yeyote yule anayeishi Tanzania atakwambi jinsi filamu zinavyotoka za kumwaga(nyingi mno) karibu kila siku iendyo kwa Mungu lakini kwa mtazamo tu soko la Tanzania bado lipo chini sana na sizani kama kuna filamu nyingine zinafika hata katika nchi jirani za Tanzania nikimaanisha Kenya na Uganda.Je filamu hizi hazina ubora wa kutosha au unaotakiwa au nini haswaa tatizo?Ndio nawauliza Je tufanyaje kukuza soko la nchi ambazo ziko kama Tanzania???

Thursday, November 29, 2007

VIPI UNAMJUA MKALI WA KUNG-FU??

Ebwana nadhani wale makini wamekwisha gundua huyo ni nani ambaye anataka kuzungumziwa au sio?Kwa wale ambao wanaanza kujiuliza uliza hii inukuwaje tena?huyu jamaa anazungumzia mkaliwa kung-fu na wakati wako kibao wanaigiza filamu kibao,Hilo nalijua lakini watu wangu ukimzungumzia huyu ninaye mzungumzia ni kiboko,basi kama bado mnaumiza vichwa wale wenye kuwa na wasiwasi wala msipate tabu sana.Hata hivyo kabla sijawataji jina lake nikikwambia hivi nadhani utanipata,jamaa ameigiza filamu kama Shaolin temple 1&2 hiyo ni mwaka 1982 na 1983 pamoja na 3 mwaka 1986,Born to Defence nayo mwaka 1986,zingine ni kama Fist of legend(1994) na nyingine nyinngi pia Romeo must die(2000),The One na Kiss Of The Dragon mwaka 2001.Hero(2002),Fearless(2006) na The Warlords War(2007).Hizo movie sio kama nimewatajia zote watu wangu ni baadhi tu ya filamu alizocheza.Namzungumzia JET LEE na majina mengine kibao kama Lian Jie Li,Lianjie Li,Jet Li Lianjie,Jet Lee Lin-kit. Hayo yote ni majina yake. Jamaa alizaliwa tarehe 26 April 1963,huko Beijing,China.Huyo ndio mkali wa Kung Fu,Usikose habari zake pamoja na wengine wengi kwenye hii hii Blog yako kali ya filamu pamoja na waigizaji wa filamu hizo au sio.Kuwamakini kaa mkao wa kula.

Wednesday, November 28, 2007

KWELI MGANGA HAJIGANGI?

Msishtuke watu wangu sio kwamba nataka kuzungumzia ya kimethali sana,Hapana!Nilikuwa nahitaji tu na nyinyi mnipe maoni yenu ausio?kama ni kweli mganga hajigangi sijui hii unaionaje wewe. Je umekwisha iona filamu(movie) ya HITCH iliyoigizwa na muigizaji maarufu sana mwenye vipaji lukuki,kama vile uchekeshaji pia ni mwimbaji n.k.Kama bado ujanipata namzungumzia nani basi huyo niWill Smith.Kwenye hii filamu ameigiza kama mtu aliyebobea katika mambo ya uelimishaji wa muahusino ya kimapenzi.Je yeye ataweza kujiimarisha na kudumisha muhusiona yake na girlfriend wake au atabakia kuwaelimisha wengine na yeye anabakia kushangaa shangaa?Hebu tafuta na uicheck hiyo imetulia.

Tuesday, November 27, 2007

SHWARI TUJIKUMBUSHE KIDOGO

Nikizungumzia filamu au naweza sema movie ambazo zilitamba wakati fulani baadhi ya watu wanazo kumbuka wanaweza fahamu mimi nina rika gani hivi sasa.Lakini sio tabu sana hata ambao hawakuwepo muda huo wanaweza kuzitafuta movie hizo na kuziangalia zilivyokuwa zinarizisha.Ok msiwe na hofu wala na wasiwasi maana mtaanza kujiuliza ni zipi hizo movie jamaa anataka kuzungumzia.Poa unazikumbuka movie kama Commando ya Arnod,je Blood sport ambazo zilikuwa na mifululiza kadhaa(parts). Na zingine kibao ntazidi kuwakumbusha watu wanngu msikose basi au sio?/

KARIBUNI KATIKA BLOG MPYA YA FILAMU

Karibuni watu wote katika blog yenu mpya kabisa itakayokuwa inazungumzia kuhusu filamu mbalimbali pamoja na waigizaji wa filamu hizo. kama wewe ni mpenzi wa filamu mbalimbali basi sasa ondoa shaka maana mkombozi wako amekwisha wasili kwa sababu huta pitwa na habari za filamu bomba pamoja na wasanii au waigizaji wa filamu natumaini tuko pamona yap.